ADVERTISEMENT
  • About Us
  • Home
  • Contact Us
Friday, April 2, 2021
EastAfrica Herald
Advertisement
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More
No Result
View All Result
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More
No Result
View All Result
EastAfrica Herald
No Result
View All Result

Sasa waweza kununua tiketi za michezo kidigitali na Tigo Pesa

Krantz Mwantepele by Krantz Mwantepele
November 3, 2020
in Economy
0 0
0
Sasa waweza kununua tiketi za michezo kidigitali na Tigo Pesa
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

ADVERTISEMENT

Kaimu  Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Peter, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi mfumo kwa ajili ya kuwarahisishia mashabiki wa soka kununua tiketi kwa njia ya Tigo Pesa katika michezo mbalimbali itakayochezwa Uwanja wa Uhuru na Mkapa, Dar es Salaam.

 

Shukrani: “Natoa shukrani kwa @tigo_tanzania na NIDC kwa hatua ambayo wamechukua ili kumruhusu mtanzania na mwanamichezo awe na urahisi kuweza kuingia uwanjani kupata burudani.” Yusuph Singo-Mkurugenzi wa Michezo Tanzania.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo na Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data Kimtandao (NIDC), zimeungana kwa ajili ya kuwarahisishia mashabiki wa soka kununua tiketi kwa njia ya Tigo Pesa katika michezo mbalimbali itakayochezwa Uwanja wa Uhuru na Mkapa, Dar es Salaam.
Mashabiki wa soka wataanza kunufaika na huduma hiyo ya kisasa ili kuhakikisha wanapunguza msongamano wakati wa kukata tiketi kwa ajili ya kwenda kuangalia mechi za soka kwenye viwanja hivyo.
Akizungumza Dar es Salaam, Kaimu  Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Peter, alisema kuwa wameungana na NIDC kwa ajili ya kuwasaidia mashabiki wa soka kukata tiketi kwa njia ya mtandao.
Alisema kuwa mashabiki wa soka kwa sasa watakuwa wamepunguza suala la kutembea na fedha taslimu na badala yake wataanza kutumia huduma ya kukata tiketi kwa njia ya Tigo Pesa.
“Wateja wetu kwa sasa hawatapata tabu tena au kuhangaika kufanya malipo ya tiketi za michezo, kwani kupitia Tigo Pesa wanaweza kufanya malipo ya tiketi kidijitali kupitia kadi maalumu kutoka kwa washirika wetu kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data Kimtandao cha (NIDC).
“Tanzania ni moja ya nchi za kuigwa katika kufanya malipo kidijitali au kielektroniki. Kupitia malipo haya ya N-Card tumeendelea kupeperusha bendera katika nyanja ya malipo ya kidijitali,” alisema.
Afisa Uhusiano wa Kituo cha NIDC, Geophrey Mlelwa, alisema kuwa wamefurahia kuungana na Tigo kwa ajili ya kuleta mapinduzi kwenye michezo.
Alisema kuwa mashabiki wa soka watapata fursa ya kukata tiketi za kuangalia mechi mbalimbali bila tatizo lolote kuanzia sasa.
“Hii ni fursa kwa wapenzi wa michezo hasa mpira wa miguu kuweza kununua tiketi kirahisi na kwa haraka bila bugdha yoyote kupitia kadi hii maalum(N-card) ambapo watafanya malipo kupitia Tigo Pesa.” alisema Mlelwa.
Mkurugenzi wa Fedha wa  Yanga, Mfikirwa Hajji, alisema kuwa mashabiki wa Yanga watumie fursa hiyo hasa katika mechi yao dhidi ya Simba itakayochezwa Jumamosi.
Alisema mechi hiyo hukusanya mashabiki wengi zaidi na kwamba amewataka kununua tiketi zao mapema kwa ajili ya kuahudia mchezo huo.
“Hii ni fursa ya aina yake na kwamba tunawaomba mashabiki wetu waitumie kila wakati kwa kuanzia katika mechi yetu dhidi ya Simba itakayofanyika Jumamosi,” alisema.

Related

Previous Post

Vodacom pays out TZS 427.5 billion in dividends to equity shareholders.

Next Post

Benki ya CRDB yazindua kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako”

Related Posts

Tigo Pesa marks 10 years of revolutionizing the Mobile Financial Services market in Tanzania
Economy

10 years of Tigo Pesa: a journey of creating opportunities and improving Lives to millions of Tanzanians.

by Krantz Mwantepele
March 17, 2021
0

The growth of Tanzania’s economy mostly depends on the agriculture sector which has known as a backbone of our economy...

Read more
New SimBanking App to enable self-account opening, Bank CEO says

New SimBanking App to enable self-account opening, Bank CEO says

February 26, 2021
Morogoro Central Market

President Magufuli launches Morogoro Central Market

February 11, 2021
Kenya Airways Cargo Plane

Kenya Airways (KQ) makes history, converts Boeing 787 Dreamliner into cargo plane

February 8, 2021
Next Post
Benki ya CRDB yazindua kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako”

Benki ya CRDB yazindua kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako”

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

KRANTZ MWANTEPELE (CEO )

KONCEPT TV

International News

  • Home
  • About Us
  • Economy
  • Technology
  • Politics
  • Contact Us

All rights reserved © 2020 East Africa Herald - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More

All rights reserved © 2020 East Africa Herald - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Create New Account!

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In

Add New Playlist