Advertisement
Benki namba moja kwa utoaji wa Huduma za Kifedha hapa Nchini CRDB BANK Mapema leo hii wamefanya Hafla ya kuitimisha Wiki ya Huduma kwa wateja ambayo hi kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba  takribani duniani kote. 
Kwa upande wa CRDB Benki wao wameitimisha wiki hii kwa namna ya kipekee kabisa ambapo wafanyakazi wamejiunga katika makundi mbalimbali (Team ) na kufanya mashindano ya kucheza mziki ambapo katika mashindano hayo Timu mbili ziliibuka mshindi baada ya kucheza kwa ustadi mkubwa.

” Hawa wameibuka washindi kwasababu kuna vigezo tumevizingatia sisi kama Majaji kwanza tumeangalia Ushirikiano katika uchezaji wao, Utayari wa kufika kwenye jukwaa, mwonekano wao , uteuzi wa nyimbo pamoja na walivyokua wanafuata mapigo ya mziki” Alisema Jaji wa Mashindano hayo.

Aidha kwa upande mwingine Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja Bi. Yolanda Urio amezipongeza sana Timu zilizoshinda na kusisitiza kuwa lengo lilikua ni kutoa burudani lakini pia kuangalia namna gani wafanyakazi wanaweza kujiongoza katika kufanya kitu kimoja ili kuweza kufikia lengo ( DREAM TEAM) 
Ameendelea kwa kuwashukuru wateja wote wa CRDB kwa ushirikiano wanaoendelea kuonyesha na kusisitiza kuwa wapo tayari kuwahudumia wakati wowote na Mahali popote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here