ADVERTISEMENT
  • About Us
  • Home
  • Contact Us
Friday, February 26, 2021
EastAfrica Herald
Advertisement
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More
No Result
View All Result
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More
No Result
View All Result
EastAfrica Herald
No Result
View All Result

Benki ya NMB, NHIF waweka historia afya kwa wote

Isdora Kabindo by Isdora Kabindo
October 8, 2020
in East Africa
0 0
0
Benki ya NMB, NHIF waweka historia afya kwa wote
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

Afisa  Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa NHIF, Bernard Konga (kushoto) wakisanini mkataba wa uzinduzi wa Mpango wa DUNDULIZA kwa huduma za NHIF kupitia Benki ya NMB . Kulia ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi.


Afisa  Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa NHIF, Bernard Konga (kushoto) wakibadilishana  mkataba wa uzinduzi wa Mpango wa DUNDULIZA kwa huduma za NHIF kupitia Benki ya NMB . Kulia ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi.


 

Benki ya NMB na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) zimeweka historia mpya na ya aina yake nchini kwa kuanzisha utaratibu wa kipekee wa bima ya afya utakaowawezesha wananchi wengi kupata huduma hiyo kiurahisi na kwa nafuu kubwa kwa kuweka akiba kidogo kidogo kulingana na vipato vyao.

 

Historia hiyo iliandikwa jijini Dar es Salaam baada ya taasisi hizo mbili kuingia makubaliano ya kutekeleza mpango huo ambao unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa kwenye malengo ya taifa ya kuboresha rasilimali afya na upatikanaji wa tiba.

 

Mpango huo mahsusi wa huduma ya afya kwa wote ujulikanayo kwa jina la DUNDULIZA ulizinduliwa katika hafla iliyofanyika PSSSF Complex na kuhudhuriwa na viongozi na wafanyakazi wa taasisi hizo mbili pamoja na wadau mbalimbali.

 

Wakizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi Ruth Zaipuna, na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga,walisema ukubwa wa mtandao wa huduma wa benki hiyo utasaidia sana kuipeleka DUNDULIZA kwa Watanzania hasa wale wa kawaida kama wakulima na wajasiliamali. Pia walisema kuwa huduma hiyo mpya itakuwa na mchango mkubwa katika mipango ya serikali ya kuhakikisha afya bora kwa Watanzania wote kupitia bima ya afya.

 

 “NHIF wanapoingia makubaliano nasi, maana yake wataweza kuwafikia Watanzania wote kila pembe ya nchi hii kutokana na mtandao wetu mpana wa matawi na hata mtandao wa wakala wetu ambao ni wawakilishi katika huduma za kifedha. NMB ina matawi 227 na ipo katika kila wilaya na baadhi ya kata hapa nchini huku tukiwa na wakala wa benki (NMB Wakala) zaidi ya 7,000,” Bi Zaipuna aliongeza.

 

Kuhusu DUNDULIZA, alisema ni mpango unaomwezesha mwananchi kujiwekea akiba ya fedha kidogo kidogo za michango kwa ajili bima yake ya afya na hata wategemezi kupitia Benki ya NMB. Kwa utaratibu huu, alifafanua, mtu ataweza kufanikisha kuchangia mojawapo ya vifurushi vya bima ya afya vinavyotolewa na NHIF ambavyo ni Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya.

 

Kwa mujibu wa Bi. Zaipuna, Benki ya NMB imeamua kuwekeza katika mpango wa DUNDULIZA na kushirikiana na NHIF kuufanikisha kwa sababu afya bora ni mtaji kwao kama taasisi ya kifedha. Alisema upatikanaji wa tiba kwa kutumia bima ya afya badala ya akiba zilizowekwa benki ni swala la msingi si kwao tu lakini pia kwa wateja na wananchi kwa ujumla.

 

“Huu ni mpango wa kwanza na wa aina yake kutokea hapa nchini na tunafurahia kuwa wa kwanza kuweka historia hii ya kushirikiana na Serikali kupitia NHIF katika kuboresha huduma ya afya kwa Watanzania. Utaratibu huu pamoja na kupata bima ya afya pia unamjengea mwananchi utamaduni wa kujiwekea akiba kwa kutimiza malengo mbalimbali,” Bi Zaipuna alifafanua.

 

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF alisema kuwa wakati NHIF inazindua mpango wa vifurushi Novemba mwaka jana, changamoto iliyoonekana ni pamoja na uwezo wa wananchi kulipa fedha zote kwa awamu moja hatua iliyoifanya menejimenti ya mfuko huo kufungua milango na kuanza kushirikiana na wadau wa taasisi za kifedha kama Benki ya NMB ambayo ililipokea wazo la DUNDULIZA na kulifanyia kazi haraka.

ADVERTISEMENT

 

 

 

Related

Previous Post

Maisha Magic Bongo celebrates milestone of 5 Years of magic

Next Post

NMB UNVEILS PARTNERSHIP WITH UNION PAY INTERNATIONAL

Related Posts

Maalim Seif Sharif Hamad
East Africa

The first Vice President of Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad Dies at 78

by ALLY MSANGI
February 17, 2021
0

Zanzibar's First Vice President Maalim Seif Sharif Hamad died earlier today while receiving treatment at Muhimbili National Hospital in Dar-es-salaam....

Read more
Morogoro Central Market

President Magufuli launches Morogoro Central Market

February 11, 2021
Amka na tigo

Tigo gives every customer FREE 10 minutes every day

February 11, 2021
African Court Judge

Justice Imani Aboud Appointed to African Court on Human and Peoples’ Rights

February 10, 2021
Next Post
NMB UNVEILS PARTNERSHIP WITH UNION PAY INTERNATIONAL

NMB UNVEILS PARTNERSHIP WITH UNION PAY INTERNATIONAL

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

KRANTZ MWANTEPELE (CEO )

KONCEPT TV

International News

  • Home
  • About Us
  • Economy
  • Technology
  • Politics
  • Contact Us

All rights reserved © 2020 East Africa Herald - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More

All rights reserved © 2020 East Africa Herald - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Create New Account!

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In

Add New Playlist