ADVERTISEMENT
  • About Us
  • Home
  • Contact Us
Friday, February 26, 2021
EastAfrica Herald
Advertisement
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More
No Result
View All Result
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More
No Result
View All Result
EastAfrica Herald
No Result
View All Result

Benki ya NMB yapongezwa kwa kutoa ahueni wakati wa COVID-19

Isdora Kabindo by Isdora Kabindo
September 28, 2020
in Economy
0 0
0
Benki ya NMB yapongezwa kwa kutoa ahueni wakati wa COVID-19
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter



Serikali na wadau mbalimbali wameipogeza Benki ya NMB kwa msaada wake mkubwa wakulisaidia Taifa na wateja wake kukabiliana na changamoto za janga la COVID-19 ambalo athari zake kiuchumi na kibiashara zinaendelea kuitikisa dunia.

ADVERTISEMENT

 

Pongezi hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha wakati wa hafla ya Mtandao wa Wateja Wakubwa wa Benki hiyo ‘NMB Executve Network’ uliyowaleta pamoja wateja zaidi ya 100 wa Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa mitatu ikiwemo Tanga na Kilimanjaro.


C:\Users\elizabeth.ikengo\AppData\Local\Microsoft\Windows\INetCache\Content.Word\N 2.jpg

Wafanyabiashara wakubwa ambao ni wateja wa Benki ya NMB Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki hiyo kwenye hoteli ya Gran Melia jijini Arusha kujadili mikakati ya kuboresha ushirikiano.

 

NMB ilitangaza unafuu wa ulipaji mikopo kwa wateja wake mwezi Mei mwaka huu, kupitia likizo ya marejesho ya mikopo yao na wengine wakiongezewa muda wa kulipa mikopo hiyo ili kuwasaidia kukabiliana na madhara yaliyoletwa na COVID–19 katika biashara zao.

 

 Akizungumza wakati wa hafla hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Longido – Frank Mwaisumbe alisema NMB iliwasaidia sana wateja wake na imeendelea kuwa nao karibu wakati wote wa kipindi cha COVID-19 na wao kama Serikali wanawapongeza kwa hilo. Ni jambo kubwa hasa kwa Sekta ya Utalii ambayo imeathiriwa sana na COVID-19. Siyo hivyo tu, Frank vilevile aliipongeza Benki hiyo kwa utaratibu wake wa kukutana na wateja jambo ambalo alisema linasaidia kuboresha mahusinao kati ya Benki na wateja wao.

C:\Users\elizabeth.ikengo\AppData\Local\Microsoft\Windows\INetCache\Content.Word\N 3.jpg

 Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi wa Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki hiyo kwenye hoteli ya Gran Melia jijini Arusha.


Naye Afisa Mkuu wa Huduma Jumuishi wa NMB – Nenyuata Mejooli alisema, Benki ya NMB ilitoa ahuweni kwa wateja wake ili kuhakikisha shughuli zao zinastahimili misukosuko ya COVID-19 ikiwemo kubadilisha mfumo wa urudishaji mikopo kulingana na ukubwa wa athari.

 

Wakati huohuo, Nenyuata, aliwapongeza wateja wao kwa ukakamavu waliouonyesha kipindi cha COVID-19 na kuahidi kuendelea kuwa nao bega kwa bega. “Tunaelewa katika kipindi hiki,biashara kama utalii na sekta ya hoteli zilipata changamoto. Sisi kama NMB tumehakikisha tupo karibu zaidi nanyi wateja wetu ili kuhimili changamoto hizo zilizojitokeza,” aliongeza.

 

Wiki hiyohiyo, NMB pia iliweza kuwakutanisha wateja wadogo na wa kati walioujiunga na mtandao maalumu wa ‘NMB Business Club’ na kuwapa elimu ya masuala ya kibenki ikiwemo mifumo mipya ya malipo kupitia NMB Mkononi, Mastarcard QR pamoja na huduma zingine za Benki kama Bima (NMB Bancassuarance).

C:\Users\elizabeth.ikengo\AppData\Local\Microsoft\Windows\INetCache\Content.Word\DSC_1490.jpg

Washiriki wa kongamano la wafanyabiasha Wadogo na wa Kati waliojiunga na Mtandao wa NMB Business Club kutoka Arusha, Moshi na Tanga wakiwa katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.


C:\Users\elizabeth.ikengo\AppData\Local\Microsoft\Windows\INetCache\Content.Word\DSC_1359.jpg

Mwakilishi wa kiwanda cha ngozi cha Tanneries kutoka Himo Wilaya ya Moshi – France Sawerio kulia,akitoa maelezeo kwenye maonesho ya bidhaa anazo zitengeneza,wakati Viongozi wa Benki ya NMB walipo tembelea banda lake wakati wa Kongamano la wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (NMB Business Club), lililofanyika katika ukumbi wa Kuringe – mjini Moshi.

Tangu kuanzishwa kwa NMB Business Club miaka sita iliyopita, mtandao huo upo kwenye Mikoa ya; Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Mtwara, Mbeya na Dodoma huku washirika wake wakiwa zaidi ya 600.

 

Related

Previous Post

Experts outline East Africa’s post-pandemic recovery strategy at ACCA webinar

Next Post

Benki ya NMB yashiriki mkutano wa vijana wa Umoja wa Mataifa Arusha

Related Posts

New SimBanking App to enable self-account opening, Bank CEO says
Economy

New SimBanking App to enable self-account opening, Bank CEO says

by Krantz Mwantepele
February 26, 2021
0

CRDB Bank has announced the launch of its enhanced “SimBanking” mobile banking application and USSD to provide customers with state-of-the-art...

Read more
Morogoro Central Market

President Magufuli launches Morogoro Central Market

February 11, 2021
Kenya Airways Cargo Plane

Kenya Airways (KQ) makes history, converts Boeing 787 Dreamliner into cargo plane

February 8, 2021
M-Pesa customers

Vodacom M-Pesa customers reap 3.92bn interest

February 2, 2021
Next Post
Benki ya NMB yashiriki mkutano wa vijana wa Umoja wa Mataifa Arusha

Benki ya NMB yashiriki mkutano wa vijana wa Umoja wa Mataifa Arusha

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

KRANTZ MWANTEPELE (CEO )

KONCEPT TV

International News

  • Home
  • About Us
  • Economy
  • Technology
  • Politics
  • Contact Us

All rights reserved © 2020 East Africa Herald - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More

All rights reserved © 2020 East Africa Herald - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Create New Account!

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In

Add New Playlist