Advertisement
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Ltd, Margaret Karume (kulia) pamoja na Mkurugenzi  wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa benki hiyo, Bw. Gift Shoko (wa pili kulia) wakiongoza matembezi ya uzinduzi wa matawi mawili mapya ya benki hiyo mkoani Arusha. Matawi hayo ni  Clock Tower iliyopo Fire Road katika jengo la TFA, pamoja na tawi la Sokoine iliyopo barabara ya Sokoine, jengo la Central Plaza. 


Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Benki ya NCBA wakishiriki katika matembezi ya uzinduzi wa matawi mawili mapya ya benki hiyo mkoani Arusha. Matawi hayo ni  Clock Tower iliyopo Fire Road katika jengo la TFA, pamoja na tawi la Sokoine iliyopo barabara ya Sokoine, jengo la Central Plaza. 


Meneja wa tawi la benki ya NCBA lililopo mtaa wa Sokoine jijini Arusha,  Francis Pondo (kulia) akimkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw Richard Kwitega (kushoto) katika tawi hilo katika tukio la uzinduzi wa tawi hilo lililoendana na matembezi mafupi. Pamoja naye ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Ltd, Margaret Karume (wa pili kulia) na Mkurugenzi  wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa benki hiyo, Bw. Gift Shoko (wa tatu kulia).


Wafanyakazi na wakaazi wa jiji la Arusha wakishiriki katika matembezi ya kuikaribisha benki ya NCBA mkoani Arusha  ambapo benki hiyo imezindua  matawi mawili mapya mkoani hapo. Matawi hayo ni  Clock Tower iliyopo Fire Road katika jengo la TFA, pamoja na tawi la Sokoine iliyopo barabara ya Sokoine, jengo la Central Plaza. 

Matembezi hayo yalishereheshwa  na bendi ya Polisi.Wafanyakazi na wakaazi wa jiji la Arusha wakishiriki katika matembezi ya kuikaribisha benki ya NCBA mkoani Arusha  ambapo benki hiyo imezindua  matawi mawili mapya mkoani hapo. Matawi hayo ni  Clock Tower iliyopo Fire Road katika jengo la TFA, pamoja na tawi la Sokoine iliyopo barabara ya Sokoine, jengo la Central Plaza. 

Matembezi hayo yalishereheshwa  na bendi ya Polisi.Wafanyakazi na wakaazi wa jiji la Arusha wakishiriki katika matembezi ya kuikaribisha benki ya NCBA mkoani Arusha  ambapo benki hiyo imezindua  matawi mawili mapya mkoani hapo. Matawi hayo ni  Clock Tower iliyopo Fire Road katika jengo la TFA, pamoja na tawi la Sokoine iliyopo barabara ya Sokoine, jengo la Central Plaza. 

Matembezi hayo yalishereheshwa  na bendi ya Polisi.

 

Arusha. Benki ya NCBA Tanzania Limited (NCBA) imefanya uzinduzi wa kihistoria wa matawi yao mawili mapya jijini Arusha leo tarehe 19 Septemba, 2020. 

Matawi haya mawili mapya ya Arusha ni Tawi la Clock Tower lililopo Fire Road, Jengo la TFA na Tawi la Sokoine lililopo barabara ya Sokoine, Central Plaza ghorofa ya chini.


Benki ya NCBA, ni muunganiko wa hiari kati ya NIC (T) Limited na CBA Bank (T) Limited ambapo huduma rasmi za taasisi hii mpya ya Kifedha zilianza Julai 8, 2020 baada ya idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania. 

Matawi mawili ya NCBA Bank mkoani Arusha ni kati ya matawi 12 ya NCBA Bank kote nchini, mengine yakiwa Dar es Salaam, Zanzibar na Mwanza. 

Wateja wote wapo huru kutembelea tawi lolote lile la NCBA Bank ili kupata huduma zile zile bora kwa kiwango cha kimaitaifa, iwe mjini Arusha ama katika miji mingine hapa nchini. Pia kufuatia muunganiko huo, wateja wana uhuru na urahisi wa kutumia machine yoyote ile ya ATM yenye nembo ya NCBA Bank ukiwa Mwanza, Arusha, Zanzibar, Dar es salaam ama katika nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda, na Ivory Coast. 

NCBA Bank imewahakikishia wateja kuwa wataendelea kupata huduma bora za kibenki kwa kiwango cha kimataifa kwa njia za kidigitali au kwa kutembelea ATM yoyote na matawi yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here