ADVERTISEMENT
  • About Us
  • Home
  • Contact Us
Tuesday, March 30, 2021
EastAfrica Herald
Advertisement
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More
No Result
View All Result
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More
No Result
View All Result
EastAfrica Herald
No Result
View All Result

Benki Ya Crdb Yazindua Tawi La Kisasa Linalotembea Wilayani Mlele, Katavi

Isdora Kabindo by Isdora Kabindo
August 26, 2020
in East Africa
0 0
0
Benki Ya Crdb Yazindua Tawi La Kisasa Linalotembea Wilayani Mlele, Katavi
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Benki ya CRDB imeendelea na jitihada za kupanua wigo wake wa kuwahudumia wateja na kufikisha huduma za benki hiyo kwa Watanzania walio wengi kwa kuzindua tawi jipya na la kisasa linalotembea “Mobile branch” katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mh. Juma Zubier Homea ameipongeza Benki ya CRDB kwa uzinduzi wa tawi hilo linalotembea katika wilaya ya Mlele huku akisema tawi hilo litasaidia kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi katika wilaya hiyo na wilaya za jirani.

Mkuu wa mkoa huyo alisema wilaya hiyo ya Mlele ni moja ya kiungo muhimu cha uchumi katika mkoa huo wa Katavi, hivyo uwepo wa tawi hilo utasidia upatikanaji wa huduma za kifedha na kuongeza fursa nyingi za maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Katavi.

“Niwapongeze Benki ya CRDB kwa kuendelea kuonyesha uzalendo wenu kwa kubuni njia mbalimbali za kufikisha huduma kwa Watanzania, tawi hili litakwenda kuwa kichocheo kwa maendeleo ya wana mlele na Katavi kwa ujumla,” alisema Mh. Homea huku akibainisha tawi hilo linalotembea linaonyesha ubunifu wa hali ya juu na kuyataka mabenki mengine yaweze kuiga mfano wa Benki ya CRDB kwa kutumia njia mbadala kufikisha huduma kwa wateja.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Juma Zuberi Homera akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi linalotembea “Mobile Branch 19” la Benki ya CRDB katika mji wa Majimoto wilayani Mlele Mkoani Katavi. Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Benki ya CRDB, Bw.Denis Mwoleka, Kulia wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Rachel Kassanda, na Kulia wa pili ni Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano na Mahusiano, Emmanuel Kiondo. Uzinduzi huo uliambatana Benki ya CRDB kukabidhi msaada wa pikipiki 7 zenye thamani ya Milioni 17.5 kwa vyama vya ushirika vya wilaya za Mkoa wa Katavi

Homela aliwataka wananchi wa Mlele na Vitongoji vyake sasa kuchangamkia fursa mbalimbali zitolewazo na Benki ya CRDB katika kukuza uchimi na uzalishaji kwa mtu mmojamoja na hata vikundi kwa ujumla. Hasa katika kujipatia mikopo nafuu itolewayo na benki hiyo katika kuinua shughuli za kilimo, biashara na ufugaji. 

Katika uzinduzi huo Benki ya CRDB pia ili mkabidhi mkuu wa mkoa wa Katavi msaada wa pikipiki 7 zenye thamani ya shilingi milioni 17.5 kwa ajili ya kusaidia shughuli za vyama vya ushirika katika wilaya za Mkoa wa Katavi. Msaada huo ni sehemu ya sera ya Benki ya CRDB ya kusaidia jamii (CSR Policy) inayoelekeza matumizi ya asilimia 1% ya faida ya Benki kila mwaka katika kuchangia maendeleo na ustawi wa jamii.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki hiyo, Tully Mwambapa, Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo alisema uzinduzi wa tawi hilo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo katika kusaidia jitihada za serikali ya awamu ya tano ya kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi ili kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kurahisisha ufanikishaji wa miamala ya kifedha kwa wananchi mmoja mmoja na biashara.

ADVERTISEMENT

Kiondo alisema uzinduzi huo wa tawi hilo linalotembea unaenda sambamba na utoaji huduma kupitia njia mbalimbali mbadala za kidijitali ili kuongeza urahisi na unafuu wa upatikanaji wa huduma kwa wateja. Huduma hizo ni pamoja na CRDB Wakala, SimBanking, SimAccount, na huduma kupitia mtandao ‘Internet Banking’.

 

“Njia hizi za kidijitali za utoaji huduma zinamuwezesha mteja kufanya miamala yake yote popote pale alipo na wakati wote masaa 24” alisisitiza Kiondo huku akibainisha kuwa benki katika mkoa wa Katavi benki hiyo pia inatoa huduma kupitia CRDB Wakala zaidi ya 60.

Akizungumza juu ya huduma zinazotolewa na tawi hilo linalotembea, Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Benki ya CRDB, Denis Mwoleka alisema wateja watapata huduma zote kuanzia kufungua akaunti, kuweka fedha, huduma za fedha za kigeni, pamoja na maombi ya mikopo. 

Mwoleka alibainisha kuwa tawi hilo litakuwa likitoa huduma kwa siku 6 za wiki kuanzia jumatatu mpaka jumamosi huku  huduma za ATM zikipatikana siku zote za wiki masaa 24.

Benki ya CRDB inaongoza nchini kwa kuwa na mtandao mpana wa matawi zaidi ya 260, CRDB Wakala zaidi ya 15,000, ATM zaidi ya 550, mashine za manunuzi (PoS) zaidi ya 1,500. Benki hiyo pia inatoa huduma kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja kinachotoa huduma saa 24/7.


Related

Previous Post

NMB Yasogeza huduma zake Mlimba

Next Post

Kimei aiteka Vunjo, Moshi.

Related Posts

Tigo Pesa and Visa partner to enable Tanzanian consumers move funds quickly and securely  through Visa Direct
East Africa

Tigo Pesa and Visa partner to enable Tanzanian consumers move funds quickly and securely through Visa Direct

by Krantz Mwantepele
March 30, 2021
0

Tanzania’s leading digital lifestyle company, Tigo has today announced a partnership with Visa Inc. that will extend real-time access to...

Read more
Tigo customers win cash prizes as part of campaign to mark 10years of Tigo Pesa

Tigo customers win cash prizes as part of campaign to mark 10years of Tigo Pesa

March 20, 2021
Tigo Pesa marks 10 years of revolutionizing the Mobile Financial Services market in Tanzania

Tigo Pesa marks 10 years of revolutionizing the Mobile Financial Services market in Tanzania

March 8, 2021
Maalim Seif Sharif Hamad

The first Vice President of Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad Dies at 78

February 17, 2021
Next Post
Kimei aiteka Vunjo, Moshi.

Kimei aiteka Vunjo, Moshi.

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

KRANTZ MWANTEPELE (CEO )

KONCEPT TV

International News

  • Home
  • About Us
  • Economy
  • Technology
  • Politics
  • Contact Us

All rights reserved © 2020 East Africa Herald - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • East Africa
  • Politics
  • Economy
  • Technology
  • Entertainment
  • Sports
  • More

All rights reserved © 2020 East Africa Herald - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Create New Account!

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In

Add New Playlist