November 30, 2020

EastAfrica Herald

East African Views on Global News.

Benki Ya Crdb Yatoa Mikopo Ya Bilioni 500 Kwa Akinamama


Mwanasheria
wa Manispaa ya Ubungo, Kissa Mbila ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
kongamano la wanawake wajasiriamali
akipokelewa na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mbezi Luis jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd.

Mgeni
rasmi Mwanasheria wa Manispaa ya Ubungo, Kissa Mbila (katikati), kabla
ya kufungua kongamano la wajasiriamali.


Meneja
wa Benki ya CRDB Tawi la Mbezi Louis, Agness Kisinini, akizungumza
wakati wa kongamano wa wanawake wajasiriamali.

Washiriki.

Meneja wa Benki ya
CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd, akitoa hotuba yake kabla ya
kumakarisha mgeni rasmi kufungua kongamano la wanawake wajasiriamali
lililoandaliwa na benki hiyo.

Washiriki wa kongamano hilo.


Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.

Meneja wa Benki ya
CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd, akitoa hotuba yake kabla ya
kumakaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano la Wanawake Wajasiriamali wa Manispaa ya Ubungo lililoandaliwa na Benki ya CRDB.

Mwanasheria
wa Manispaa ya Ubungo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano wa
wajasiriamali wanawake, Kissa Mbila, akifungua kongamano hilo.


Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika kongamano hilo.

Mwanasheria wa Manispaa ya Ubungo, Kissa Mbila, akiteta jambo na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya CRDB, Badru Idd.

Kucheza muziki.

Meneja Mikopo wa Benki ya CRDB Tawi la Mbezi Louis, Isaack Msema, akijibu maswali ya washiriki wa mafunzo hayo.

Mjasiriamali
wa vinywaji Doreen Simfukwe, akiuliza shwali wakati wa kongamano la
Wanawake Wajasiriamali wa Manispaa ya Ubungo lililoandaliwa na Benki ya
CRDB.

Neema Tarimo akiuliza swali wakati wa kongamano la Wanawake Wajasiriamali wa Manispaa ya Ubungo.

Mgeni
rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano
hilo waliokabidhiwa vyeti kwa ajili ya kuongoza katika kuweka mialama
mikubwa katika akaunti ya CRDB Malkia.Benki ya CRDB imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali wa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam kupitia huduma ya CRDB Malkia. 


Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya CRDB, Badru Idd, alisema kuwa benki hiyo imeweza kutoa mikopo ya karibu Shilingi Bilioni 500 huku zaidi ya akinamama 25,000 wakinufaika na mikopo hiyo.


Aidha aliongeza kuwa gharama ya kufungua akaunti ya CRDB Malkia imepungua kutoka shilingi 50,000 hadi 5,000.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Mwanasheria wa manispaa hiyo, Kissa Mbila, ameipongeza Benki ya CRDB kwa kutoa mikopo nafuu yenye riba ya asilimia 14 kwa vikundi vya akinamama kupitia CRDB Malkia.

“Kupungua kwa riba inapunguza mzigo mkubwa wa marejesho kwa wanawake na kuwafanya kuwa na fedha nyingi kwa ajili ya uwekezaji katika biashara zao na hivyo kunufaika  zaidi,”

“Kupitia kikundi ni rahisi mwanamke kupata mkopo wa kuanzisha biashara na anapofanya vizuri inamuwezesha kupata mkopo binafsi kwa ajili ya kuboresha biashara yake zaidi”. Alisema Mbila.

Aidha aliwahamasisha wanawake wa Ubungo wachangamkie fursa hii kwani si benki zote wanafanya hili, unapokuwa unapata mkopo wenye riba ya asilimia 14 ni mkopo ambao una asilimia ndogo sana ukilinganisha na mikopo mingine, mwanamke akijimudu kiuchumu jamii nzima inakuwa iko katika hali nzuri kiuchumi.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mbezi Louis, Agness Kisinini, alisema kuwa “Akaunti ya Malkia inamuwezesha mwanamke kuweza kufikia malengo yake, ni kaunti ambayo inakusaidia kuweka hela kidogokidogo kutokana na kipato chako”.

“Aidha aliwataka wanawake wanaotaka kutimiza malengo yao kupitia akaunti ya CRDB Malkia wajiunge sasa kwa kuwa akaunti hiyo ni salama na  mtu akiweka fedha zake anaweza kuzipata wakati wowote tofauti na utunzaji wa hela kwa kutumia kijumbe jambo ambalo anaweza kutoweka na fedha kwa wale wanaocheza upatu.